Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: limemnukuu Demeke Mekonnen akisema hayo kwa mnasaba wa mwaka wa 10 tangu kuanzishwa mradi mkubwa wa ujenzi wa bwawa la al Nahdha na kuongeza kuwa, mradi huo si kwa ajili ya vizazi vijavyo tu, bali kukamilishwa kwake ni sawa na kulinda haki ya kujitawala taifa zima la Ethiopia.
Amesema, mradi huo utailetea Ethiopia ustawi na maendeleo makubwa na kuongeza kuwa, asilimia 86 ya maji ya Mto Nile ni mali ya nchi yake, hivyo ni haki ya Ethiopia kutumia vizuri rasilimali yake hiyo muhimu.
Kabla ya hapo nchi mbili za Sudan na Misri zilikuwa zimetangaza kwamba zina nia ya kulipeleka faili la mzozo wa Bwawa la al Nahdha kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
342/